Chuja:

wasichana

©UNICEF/Bernardino Soares

Wanawake wanaotumia intaneti ni asilimia 57 tu duniani ikilinganishwa na asilimia 62 ya wanaume-ITU

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wasichana katika tasnia ya Habari na teknolojia ya mawasiliano ICT muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU umesema fursa na usalama mtandaoni ambayo ndio maudhui ya siku ya mwaka huu ni ufunguo wa kukiingiza kizazi kijacho cha wasichana katika Habari na teknolojia ya mawasiliano.

Sauti
2'50"
UN News

Sawa Wanawake Tanzania yakabidhi majengo mawili kwa serikali ya Tanzania kusaidia vita dhidi ya unyanyasaji wa watoto

Mwishoni mwa mwaka jana 2021, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF lilisema mwaka huo ulikuwa wa machungu na ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto. Ingawa taarifa ya UNICEF ililenga katika mizozo ya muda mrefu na ile mipya ni wazi kuwa matukio ya ukiukwaji wa haki za watoto na unyanyasaji dhidi yao, unaendelea kujidhihirisha katika maeneo mbalimbali duniani.

Sauti
4'2"

14 Desemba 2021

Hujambo na karibu kusikiliza jarida msomaji wako ni Flora Nducha anayekuletea mambo kadha wa kadha ikiwemo

Ripoti inayoonesha kuongeza kwa njaa barani Afrika huku ukanda wa Afrika Mashariki ukiongoza kwa asilimia 44. 

Wakimbizi wa DRC walioko nchini Uganda wameanza kurejea makwao kwa hiyari.

Sauti
13'9"
UNICEF/Sigfried Modola

Programu ya UNICEF Turkana yawasaidia watoto wa kike kurejea shuleni

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto duniani UNICEF kwa kushirikiana na serikali ya Kenya wanaendesha programu maalum ya “Elimisha mtoto” inayowachagiza wazazi na watoto wa kike waliocha shule wakati wa janga la corona au COVID-19 na kwa sababu ya mimba za utotoni, na sababu nyingine kurejea shuleni. 
 
(TAARIFA YA FLORA NDUCHA) 
Nattss…. 

Sauti
2'46"
Mwanafunzi mwenye uoni hafifu akifanya mazoezi ya kutumia mashine ya nukta nundu kwenye shule ya watu wasioona ya Al-Noor  huko Mogadishu nchini Somalia.
UN Photo/Ilyas Ahmed)

MINUSCA yafanikisha wasichana bubu na viziwi kujikwamua

Msichana Theresa Kpana nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ambaye ni bubu na kiziwi baada ya kushindwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu kutokana na ukosefu wa miundombinu kwa watu kama yeye, sasa amechukua hatua ya kuunda kikundi cha wasichana 60  viziwi na bubu ili hatimaye wapate stadi za maisha na haki zao zilindwe kwa kuwa hivi sasa mustakabali wao uko mashakani.

Sauti
2'22"