Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini China, limetangaza hii leo kuwa mnamo tarehe 12 mwezi Desemba mwaka jana 2019, lilitia saini makubaliano ya msaada wa dola milioni mbili na Shirika la maendeleo la China, CIDCA ili kuwasaidia watu walioathirika na kimbunga Idai nchini Zimbabwe.