Chuja:

Addis Ababa

23 APRILI 2020

Katika jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

Umoja wa Mataifa wasema teknolojia ya mawasiliano imedhihirisha umuhimu wake hasa wakati huu wa janga la virusi vya Corona au COVID-19 na hivyo kuhimiza wasichana wengi wawezeshwe kuingia katika teknolojia hiyo ya ICT

-Vifaa na misaada kutoka kituo kikuu kilichopo Addis Ababa Ethiopia vyaleta mabadiliko kwa maelfu ya watu katika vita dhidi ya COVID-19 limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP

Sauti
11'13"

Hakuna mpito usio na msukosuko

Nyakati za mpito katika taifa katu hazikosi misukosuko, lakini hatimaye nuru inaonekana, amesema Zeid Ra’ad Al Hussein mwishoni mwa ziara yake nchini Ethiopia, nchi iliyoshuhudia mvutano wa hali ya juu kati ya serikali na wapinzani. 

Kamishna huyo wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema hayo leo mjini Addis Ababa, Ethiopia mwishoni mwa ziara yake ya siku nne nchini humo kufuatia mwaliko wa serikali.

Ametaja misukosuko hiyo kuwa ni pamoja na mvutano kati ya serikali na wapinzani wa kisiasa ambapo baadhi yao bado wamesweka rumande huku wengine wakiachiliwa huru.

Sauti
1'52"