Moto wawaacha maelfu ya wakimbizi wa Rohingya bila makazi Bangladesh: IOM
Moto mkubwa uliokumba kambi namba 11 iliyo chini ya eneo linalosimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM huko Cox's Bazar nchini Bangkadeshi jana Jumapili tarehe 5 Machi, umeathiri takriban wakimbizi 12,000 wa Rohingya, na kusababisha uharibifu mkubwa katika sehemu muhimu ya kambi hiyo kubwa zaidi ya wakimbizi duniani.