Indonesia

IFAD na kampuni ya Mars zachukua hatua kunusuru wakulima wa kakao na walaji wa chokoleti

Mfuko wa kimataifa wa ufadhili wa ajili ya kilimo IFAD na kampuni kubwa ya kutengeneza chokoleti duniani Mars zimeshikamana kuchukua hatua kukabiliana na uhaba wa zao la kakao ambalo ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa kiburudisho kinachopendwa kila kona ya dunia, chokoleti. 

22 APRILI 2020

Leo katika jarida la Umoja wa Mataifa Flora Nducha anakuletea

Sauti -
12'44"

Guterres aelezea kusikitishwa na vifo kutokana majanga Indonesia huku akitoa mshikamano kwa mamlaka.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea kusikitishwa kwake na vifo, uharibifu wa mali na kufurushwa kwa watu kufuatia mafuriko na tetemeko la ardhi huko Sentani, Jayapura na Papua magharibi mwa jimbo la Tenggara nchini Indonesia.

Mkimbizi kutoka Afghanistan apata fursa ya kuonyesha uwezo wake wa ubunifu wa mitindo ya nguo Indonesia

Mradi wa Benang wa mavazi ya mitindo nchini Indonesia unawapatia fursa adimu wakimbizi ambao si tu fursa kupata ajira ni adimu bali pia katika maeneo mengine hawaruhusiwi kufanya kazi. Arnold Kayanda na ripoti kamili.

Sauti -
1'35"

Kampuni ya mitindo mjini Jakarta inawapa nafasi wakimbizi kujifunza biashara na kufikia ndoto zao

Mradi wa Benang wa mavazi ya mitindo nchini Indonesia unawapatia fursa adimu wakimbizi ambao si tu fursa kupata ajira ni adimu bali pia katika maeneo mengine hawaruhusiwi kufanya kazi. 

Waliokufa Indonesia kutokana na Tsunami sasa ni 281- OCHA

Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na tsunami iliyokumba  maeneo ya mwambao mwa kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia sasa imefikia 281 na wengine zaidi ya 1,000 wamejeruhiwa. 

Wimbi kubwa la Tsunami laleta madhara makubwa Indonesia, UN yasema iko tayari kusaidia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza masikitiko yake makubwa kufuatia vifo, majeruhi na uharibifu mkubwa uliosababishwa na wimbi kubwa la tsunami lililopiga maeneo  ya pwani ya kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia jana Jumamosi.

FAO yainua wakulima wadogo wadogo Tanzania kwa kuwapa stadi za kilimo

Shirika la Chakula na kilimo duniani FAO kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania wameungana kutelekeza mradi wa kuwafundisha wakulima wadogowadogo stadi za kilimo bora. Tayari zaidi ya wataalam 1000 wanaofanya kazi katika zaidi ya wilaya 137 nchini Tanzania wamefundishwa stadi hizo katika Chuo cha wakulima cha Mkindo kilichoko Morogoro. 

Watu zaidi ya 500 wakamatwa Papua Indonesia, UN yatiwa hofu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imesema inatiwa hofu na hatua ya kukamatwa watu zaidi ya 500 waliokuwa wakiandamana kwa amani kuadhimisha siku ya taifa Papua Magharibi.

FAO kuwasaidia waathirika wa Tsunami Indonesia

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limezindua mpango utakaowasaidia  zaidi ya wakulima 70,000 wa Indonesia  pamoja na wafuga wa samaki kuweza kurudia kazi zao za zamani baada ya tetemeko la ardhi na tsunami vilivyosambaratisha mbinu za kukwamua maisha yao.