Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yasaka dola milioni 157 kusaidia wahanga wa Boko Haram

UNHCR yasaka dola milioni 157 kusaidia wahanga wa Boko Haram

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, pamoja na washirika wake katika juhudi za kutoa misaada ya kibinadamu, leo limezindua harambee ya kuchangisha dola millioni 157 kusaidia  watu  zaidi ya robo millioni ambao wameathirika  na mashambulizi ya kundi la Boko Haram katika eneo la  bonde la ziwa Chad.

Mashirika 47 ya Umoja wa Mataifa na mengine ya misaada ya kibinadamu, ambayo yameungana pamoja katika mkakati wa kikanda kusaidia wakimbizi wa Nigeria wa mwaka 2018-RRRRP yatawajikita kushughulikia mahitaji ya wakimbizi wa Nigeria 208,000 pamoja na wenyeji wao 75,000 katika nchi za Niger, Cameroon na Chad.
 
Akizindua harambee hiyo, katika mji mkuu wa Niger, Niamey, naibu kamishna wa UNHCR, Kelly T. Clements, amesema kuwa mgororo wa Boko Haram umedumu kwa muda mrefu na baado haujamalizika, na hivyo kaiomba dunia kutowasahau waathiriwa  wa mgororo huo mbaya, hususan kukiwa na  matumaini kidogo ya hali kutulia kwa kipindi kifupi kijacho.
 
Wakimbizi kutoka Nigeria wanaendelea kumiminika katika   mataifa jirani. Tangu mgogoro wa Boko Haram uanze  mwaka 2013, watu takriban millioni 2 unusu wamesambaratishwa ndani mwa nchi zao kama vile kaskazini mashariki mwa Nigeria, Cameroon, Chad na Niger.
 
Na moja ya athari za mgogoro huo ni hali inayoongezeka ya uhaba wa chakula na utapia mlo katika maeneo hayo.
Kufikia mwaka 2017 watu katika eneo la bonde la ziwa Chad walikabiliwa na shida kubwa  ya chakula.  
Audio Duration
1'53"
Photo Credit
Mtoto akiwa na hali ya utapiamlo katika kambi ya wamkimbizi wa ndani ya Assaga karibu na mji wa Diffa nchini Niger.