Jamii ya Watyaba kandoni mwa Ziwa Albert nchini Uganda yatishiwa tena na mafuriko
Wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP26 unaendelea katika huko Glosgow na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwa amewaeleza viongozi wa ulimwengu kuwa ni muhimu kuchukua hatua sasa kwani wanadamu wanajichimbia kaburi, nchini Uganda jamii ya Watyaba, mojawapo ya jamii za walio wachache wanaoishi katika viunga vya Ziwa Albert, wanapaza sauti kwa serikali na shirIka la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kuwasaidia kutokana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya uganda, tzaidi ya watu 300,000 wameathiriwa na mafuriko kote nchini Uganda.
Basi ungana na mwandishi wetu wa Uganda John Kibego ili kufahamu hali halisi katika mahojiano baina yake na Badru Kantanda, kiongozi wa Watyaba.