Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNDP Tanzania/Sawiche Wamunza

UNDP yapiga jeki juhudi za wakulima wa pilipili Tanzania

Nchini Tanzania harakati za kuondokana na umaskini zinaendelea kushika kasi mashinani zikipigiwa chepuo na Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa hatua hizo ni kilimo cha kisasa cha mboga mboga na matunda kinachoendeshwa na wanawake kupitia chama cha wakulima wa mboga na matunda nchini Tanzania, TAHA. TAHA imepatiwa msaada na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP nchini Tanzania na sasa kupitia vikundi mbalimbali, wakulima wanalima mazao ambayo yanakidhi vigezo vya kuuzwa nje ya nchi.

Sauti
5'38"
UN-Habitat/Julius Mwelu

Tunafanikiwa kuwaelimisha watu wasichafue mazingira wakati wa msimu wa mvua-Jikomboe Youth Group

Katika miji mikubwa nchini Tanzania, msimu wa mvua ni msimu unaokuja na changamoto kadha zikiwemo za magonjwa, mafuriko na uchafuzi wa mazingira kutokana na watu kutumia mwanya huo kutupa taka kwa kutegemea maji ya mvua kuzibeba taka hizo. Ni bahati mbaya kuwa baadhi ya taka hizo kama plastiki huishia katika mazingira au vyanzo vya maji na mifereji na kusababisha matatizo kwa mazingira.
Sauti
3'53"
UN News Kiswahili

Kupata utambuzi na tuzo maana yake kazi yako imeonekana na ni fursa kufanya zaidi

Shirika lisilo la kiserikali la CAMFED nchini Tanzania ni moja ya mashirika yanayopambana kuhakikisha yanachangia katika kutimiza angalau malengo machache kati ya malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs. Shirika hili kwa kiasi kikubwa limejikita katika lengo namba 4 linalozungumzia elimu bora na lengo namba 5 linazungumzia usawa wa kijinsia, yote hayo yakiwa yanalenga kutomwacha nyuma mtu yeyote katika maendeleo ya ulimwengu ifikapo mwaka 2030. 

Sauti
4'1"
UN News/ John Kibego

Kijana mkimbizi kutoka Sudan Kusini atuzwa kwa kusoma habari za Kingereza Uganda

Licha ya changamoto za ukimbizini hasa wakati huu wa COVID-1, bado kuna mianya ya tabasamu kwa vijana wakimbizi wanojitahidi kushiriki kwenye fursa chache zilizopo.

Nchini Uganda katika mji wa Hoima, kijana mkimbizi, Emmanuel Edema kutoka Sudan Kusini ametuzwa baada ya kuibuka msomaji bora wa habari za lugha ya Kingereza  kwenye mashindano yalioandaliwa na redio washirika Spice FM.

Sauti
3'42"
UN Environment/Georgina Smith

Wanawake Tanga hatujibweteki, tunajishughulisha

Wanawake 10 mkoani Tanga Tanzania wameunda kikundi cha kushirikiana kufanya shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato ambapo wanatumia zao la mkonge au katani kutengeneza bidhaa mbalimbali, shughuli ambayo imewainua kiuchumi. Stella Vuzo wa Kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC Dar es Salaam akiwa mkoani Tanga Tanzania amezungumza na mmoja wa wanawake hao. 

Sauti
3'25"