Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Kilimo bora chaimarisha kipato cha kaya Vietnam

Kilimo ni shughuli inayoleta maendeleo siyo tu kwa kijiji, eneo au taifa kwa ujumla bali pia kwa mtu binafsi na familia yake. Ni kwa kuzingatia hilo, Umoja wa Mataifa umekuwa kila mara unakipigia upatu na kukijumuisha katika ufanikishaji wa  baadhi ya  malengo ya maendeleo endelevu, kama vile malengo namba moja la kuondoa umaskini na pia namba 2 la kutokomeza njaa bila kusahau lengo namba nane  la  kazi nzuri na ukuaji wa kiuchumi na vilevile   usawa wa kijinsia ambalo ni lengo namba tano.

Sauti
2'52"
UNHCR/Antwan Chnkdji

Kutoka maisha ya dhiki hadi zulia jekundu Ufaransa

Maisha ya mtoto Zain mwenye umri wa miaka 13 ni hadithi ya kweli ya kusisimua. Yeye pamoja na familia yake waliikimbia nchi yao ya Syria zaidi ya miaka 7 iliyopita na wakaanza maisha ya mateso ukimbizini Lebanon.

Hadithi yake inaelekea kuwa na mwisho mzuri baada ya kuigiza katika filamu inayoitwa Caphernaum na ambayo hivi karibuni imepata Tuzo nchini Ufaransa.

Zain ameondoka katika mateso, ametembea juu ya zulia jekundu kuipokea Tuzo ya Cannes na kwa msaada wa UNICEF, familia yake imepatiwa makazi nchini Norway ambako ataenda kutimiza ndoto yake ya kuwa msomi.

Sauti
2'36"
UNHCR/Catherine Wachiaya

Hedhi, ndoa za umri mdogo na kutopatiwa fursa vyatukwamisha, tusikilizeni- Watoto wa kike

Leo ikiwa ni siku ya mtoto wa kike duniani, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imebisha hodi huko mkoani  Morogoro nchini Tanzania ambako watoto wa kike pamoja na mwalimu wao wamepaza sauti zao ili kuhakikisha kuwa kundi hilo haliachwi nyuma kwa visingizio lukuki. Umoja wa Mataifa unasema kuwa ahadi yake ya mwaka 2015 inayokoma mwaka 2030 inataka kila mtu ashirikishwe katika harakati za maendeleo, sasa iweje watoto wa kike waenguliwe?

Sauti
4'28"

Jamii bado inashikilia mtazamo wa kazi fulani na jinsia fulani

Licha ya hatua zilizopigwa katika usawa wa kijinsia hususan sekta ya ajira lakini bado kuna pengo kubwa katika usawa wa kijnsia katika kazi zinazohitaji stadi za kiwango cha juu. Aidha kuna kazi ambazo mtazamo wa jamii ni kuwa kazi hizo ni za wanaume au zingine zikichukuliwa kama kazi za wanawake tu. Hali ni kama hiyo kwa msichana mmoja nchini Uganda ambaye yeye amejikita katika kazi ambayo kwa muda mrefu inatazamwa kama ya wanaume. Je jamii ina mtazamo gani kuhusu nafasi anayoshikilia na je yeye binafsi anasemaje kuhusu kazi anayofanya kuonekana kama kazi ya wanaume?

Sauti
3'33"
Nansen Initiative, via UNOCHA

Mabadiliko ya tabianchi hayabagui

Mabadiliko ya tabianchi hayabagui wala hayachagui, yanakumba kila mahali na kila bara. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa athari zake ni dhahiri na kuna maeneo yaliyoahatarini zaidi mfano yale ya nchi za visiwa vidogo vinavyoendelea.

Na athari hizo si katika uchumi tuu bali katika nyanja mbalimbali kuanzia haki za binadamu na hata michezo. Fiji ni miongoni mwa mataifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea ambako kwa miongo watu wamekuwa wakifurahia fukwe za kisiwa hicho kwa kujipumzisha na hata kufanya mazoezi kwa wanamichezo.

Sauti
3'33"
UNHCR/Catherine Wachiaya

TAMWA yapigia chepuo mazingira salama shule ili hedhi isimkwamishe mtoto wa kike

Lengo namba 4 la malengoi ya maendeleo endelevu, SDGs linapigia chepuo suala la elimu kama chombo cha kumwezesha binadamu kujinasua kwenye umaskini na kuhimili mazingira  yake.

Hata hivyo lengo hhili linachambuliwa zaidi likitaka kila mwanafunzi awe wa kike au wa kiume awe katika mazingira bora ya kumwezesha kupata elimu hiyo bila kujali jinsia yake. Mathalani mtoto wa kike anapokuwa kwenye hedhi,  isiwe kikwazo cha yeye kupata mafunzo na stadi kama wanazopata wanafunzi wa kiume.

Sauti
3'20"

Kutoka kuwa wakili mahakamani hadi kuuza mkaa

Vijana! Vijana! Vijana! Umoja wa Mataifa unasema ndio mkombozi wa kizazi cha sasa na kijacho hasa katika kuepusha dunia hii na madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayochochewa na mambo kadhaa ikiwemo ukataji miti kwa ajili ya mkaa. Ni kwa kutambua hilo, kijana mmoja nchini Tanzania wakati akisoma shahada yake ya kwanza ya sheria kwenye Chuo Kikuu, alibonga bongo ya jinsi ya kuondokana na mkaa unaoharibu mazingira. Alikuja na wazo lake ambalo katika sehemu hii ya kwanza ya mahojiano na Assumpta Massoi anaelezea safari yake na anaanza kwa kujitambulisha.

Sauti
4'15"
FAO/Giulio Napolitano

Ndoa bila vyeti Burundi si ndoa tena

Mwanamke wa Burundi akielimika anaweza kujitegemea na kufanya kila kitu kujikimu kimaisha ikiwemo kujua haki zake na kuzipigania. Amesema hayo afisa habari katika wizara ya mambo ya nje ya Burundi, Sonia Niyubahwe Ines, alipozungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii. Bi.

Sauti
3'40"