Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya tabianchi hayabagui

Mabadiliko ya tabianchi hayabagui

Pakua

Mabadiliko ya tabianchi hayabagui wala hayachagui, yanakumba kila mahali na kila bara. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa athari zake ni dhahiri na kuna maeneo yaliyoahatarini zaidi mfano yale ya nchi za visiwa vidogo vinavyoendelea.

Na athari hizo si katika uchumi tuu bali katika nyanja mbalimbali kuanzia haki za binadamu na hata michezo. Fiji ni miongoni mwa mataifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea ambako kwa miongo watu wamekuwa wakifurahia fukwe za kisiwa hicho kwa kujipumzisha na hata kufanya mazoezi kwa wanamichezo.

Lakini sasa burudani na mazoezi katika fukwe hizo vieanza kuwa historia kutokana na mabadiliko ya tabia nchi , hivyo kuwalazimu baadhi ya wanamichezo wa mpira wa Raga waliotumia fukwe hizo zamani kufanya mazoezi na sasa wamekuwa wachezaji nyota Asia na Pacific, kuchukua hatua.

Wakisaidiana na wazawa katika kijiji walikotoka wachezaji hao wanapanda miti ili kuzuia eneo lililosalia lisisombwe na maji.

Katika makala hii Assumpta Massoi anafuatilia jitihada zao ungana naye.

Audio Credit
Siraj Kalyango/ Assumpta Massoi
Audio Duration
3'33"
Photo Credit
Nansen Initiative, via UNOCHA