Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hedhi, ndoa za umri mdogo na kutopatiwa fursa vyatukwamisha, tusikilizeni- Watoto wa kike

Hedhi, ndoa za umri mdogo na kutopatiwa fursa vyatukwamisha, tusikilizeni- Watoto wa kike

Pakua

Leo ikiwa ni siku ya mtoto wa kike duniani, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imebisha hodi huko mkoani  Morogoro nchini Tanzania ambako watoto wa kike pamoja na mwalimu wao wamepaza sauti zao ili kuhakikisha kuwa kundi hilo haliachwi nyuma kwa visingizio lukuki. Umoja wa Mataifa unasema kuwa ahadi yake ya mwaka 2015 inayokoma mwaka 2030 inataka kila mtu ashirikishwe katika harakati za maendeleo, sasa iweje watoto wa kike waenguliwe? sasa wanafunguka kama ambavyo wataalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa MAtaifa hivi karibuni walitaka watoto hao wapaze sauti na serikali zisikilize sauti hizo.

Audio Credit
Grace Kaneiya/Siraj Kalyango
Audio Duration
4'28"
Photo Credit
UNHCR/Catherine Wachiaya