Kilimo bora chaimarisha kipato cha kaya Vietnam
Kilimo ni shughuli inayoleta maendeleo siyo tu kwa kijiji, eneo au taifa kwa ujumla bali pia kwa mtu binafsi na familia yake. Ni kwa kuzingatia hilo, Umoja wa Mataifa umekuwa kila mara unakipigia upatu na kukijumuisha katika ufanikishaji wa baadhi ya malengo ya maendeleo endelevu, kama vile malengo namba moja la kuondoa umaskini na pia namba 2 la kutokomeza njaa bila kusahau lengo namba nane la kazi nzuri na ukuaji wa kiuchumi na vilevile usawa wa kijinsia ambalo ni lengo namba tano.
Kwa mantiki hiyo kilimo ambacho ni endelevu kimechukuliwa kwa makini nchini Vietnam ambako kimesaidia mkulima mmoja mwanamke kupata mavuno bora ya chai. Kilimo endelevu ambacho hakiharibu mazingira kimemfanya mkulima huyo NGUYEN THI THANH kuona nuru kwenye maisha yake. Je nini kimefanyika. ungana basi na Siraj Kalyango katika makala ifuatayo.