Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka kuwa wakili mahakamani hadi kuuza mkaa

Kutoka kuwa wakili mahakamani hadi kuuza mkaa

Pakua

Vijana! Vijana! Vijana! Umoja wa Mataifa unasema ndio mkombozi wa kizazi cha sasa na kijacho hasa katika kuepusha dunia hii na madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayochochewa na mambo kadhaa ikiwemo ukataji miti kwa ajili ya mkaa. Ni kwa kutambua hilo, kijana mmoja nchini Tanzania wakati akisoma shahada yake ya kwanza ya sheria kwenye Chuo Kikuu, alibonga bongo ya jinsi ya kuondokana na mkaa unaoharibu mazingira. Alikuja na wazo lake ambalo katika sehemu hii ya kwanza ya mahojiano na Assumpta Massoi anaelezea safari yake na anaanza kwa kujitambulisha.

Audio Credit
Siraj Kalyango/Assumpta Massoi/ Iddi Hamisi
Audio Duration
4'15"
Photo Credit
Mradi wa kutengeneza mkaa wa kupikia utokanao na taka badala ya kukata miti na kuchoma mkaa. (picha:SEEDS)