Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Mamia ya wakimbizi waliokuwa Burundi warejea makwao: UNHCR

Mwezi mmoja baada ya machafuko ya kisiasa nchini Burundi kulikosababisha kuzorota kwa ustawi wa kijamii na kiucumi husuani katika jiji la Bujumbura, wakimbizi waliokuwa wamejihifadhi nchini humo wameliomba shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR kuwarejeseha makwao huku wengine wakitaka kupelekwa sehemu zenye usalama zaidi.

#PKDAy: Sasa wanawake wanahitajika zaidi kwenye ulinzi wa amani: Edith

Ikiwa leo ni siku ya walinda amani duniani, Umoja wa mataifa unaendelea kupigia chepuo harakati za kuimarisha uwezo wa vikosi vyake kwa kuwapatia vifaa vya kisasa na watendaji wenye stadi za kutosha kuweza kuhimili changamoto ziibukazo kwenye medani. Sanjari na hilo ni kuimarisha uwepo wa wanawake wakati huu ambapo wanawake kwenye mizozo hukabiliwa na shida nyingi ambazo penginepo zinaweza kukabiliwa vizuri na wanawake wenzao.

Harakati za UNICEF kuwasaidia wasichana kukabiliana na changamoto za hedhi Tanzania

Nchini Tanzania Shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF katika harakati za kukabiliana na usafi wakati wa hedhi, mwaka 2009 lilifanya utafiti ambao ulionyesha kwamba asilimia 11 ya shule 2,697 binafsi na za umma katika wilaya 16 ndio zenye vyoo vinavyokidhi angalau vigezo vya kuwezesha kujisafi ilhali  asilimia 9 vilkzingatia usafi huku asilimia moja tu vikiwa na sabuni.

Hali ya kibinadamu ya wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania

Burundi! tangazo la tarehe 27 la mahakama ya kikatiba nchini humo kumruhusu Rais Pierre Nkurunzinza kuwania kwa mara tatu nafasi ya Urais kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi sambamba na jaribio la mapinduzi lililofeli, vimeibua mzozo wa kisiasa na kibinadamu na maelfu ya wananchi wamekimbilia nchi jirani ikiwemo Tanzania. Hali ya kibinadamu inazorota huko kila uchao, kipindupindu kikiripotiwa, halikadhalika vifo, huku huduma za uzazi nazo mashakani. Je nini kinaendelea? Ungana na Joseph Msami kwenye makala hii.

Muziki unaleta mabadiliko katika jamii

Muziki ni sanaa ambayo kwayo iwapo itatumiwa vizuri italeta mabadiliko siyo tu kwa jamii ambayo inasikiliza bali pia kwa watunzi na waimbaji wenyewe. Hata hivyo kwa nchi zinazoendelea ikiwemo zile za Afrika Mashariki bado manufaa kutokana na muziki  yanasalia changamoto kutokana na ukosefu wa elimu ya kutosha kwa wasanii kuhusu haki zao hususan hakimiliki jambo ambalo sasa shirika la Umoja wa Mataifa la hakimiliki, WIPO linapigia chepuo.

Wadau wa kibinadamu wahaha kuhusu hatma ya wakimbizi wa Burundi

Takriban raia wa Burundi 100,000 wamekimbilia Tanzania, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo tangu machafuko yaibuke mwishoni mwa mwezi Aprili. UNHCR, nchi zinazowapa hifadhi na wadau kwenye ukanda, wanajitahidi kuwapa usaidizi na mahitaji yao ya kimsingi.

Wengi wa wanaokimbilia Tanzania wamewasili kwenye rasi ya Kagunga, kijiji kimoja kilichojitenga kwenye ufukwe wa Ziwa Tanganyika, ambako rasilmali ni adimu. Kutoka hapo, wanasafirishwa kwa feri hadi kwenye uwanja wa michezo wa Kigoma, ambako watapewa chakula, makazi, pamoja na maji safi na huduma za kujisafi.

Wakimbizi zaidi wa Burundi wawasili Uvira

Tangu kuanza kwa mzozo wa kisiasa nchini Burundi, tarehe 25 Aprili, siku ambapo rais Pierre Nkurunziza ametangazwa kuwa mgombea rais wa chama tawala, zaidi ya watu 100,000 wamekimbia makwao na kutafuta hifadhi kwenye nchi jirani, ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, ni zaidi ya wakimbizi 9,000 waliofika kwenye eneo la Uvira, Kivu Kusini.

Wakati UNHCR inaandaa eneo maalum kwa kuwapiatia hifadhi, jamii iliyopo Uvira imekubali kuwapokea wakimbizi hawa.

Sakata Burundi, mwanamke ajifungulia kwenye boti, majaliwa yake sasa ni usaidizi

Athari ya sintofahamu ya kisiasa inayoendelea nchini Burundi kufuatia bunge la nchi hiyo kumtangaza Rais Pierre Nkurunzinza kuwania nafasi ya Urais kwa awamu ya tatu, imeendelea kuongezeka na hata kugusa vizazi tarajiwa nchini humo. Mathalani wanawake wajawazito wamejikuta katika mazingira hatarishi siyo tu kwao bali pia watoto wao wanaojifungua na hata kuweka njia panda matarajio ya familia kuongeza uzao duniani.

Huduma za usaidizi zasonga mbele Nepal.

Nchini Nepal, wakati tetemeko la awamu ya pili likitibua matumaini ya raia ya kurejea katika hali ya kawaida baada ya lile la mwezi Aprili ambalo lilisababisha vifo vya maelfu ya watu, mashirika ya Umoja wa Mataifa sasa yanahaha kufanya tathimini za mahitaji kwa ajili ya usaidizi.

Mashirika hayo yakiongozwa na lile la mpango wa chakula duniani WFP yanakusanya taarifa toka kwa waathirika nakuangalia viwango vya madhara kama anavyosimulia Grece Kaneiya katika makala ifuatayo.