Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wadau wa kibinadamu wahaha kuhusu hatma ya wakimbizi wa Burundi

Wadau wa kibinadamu wahaha kuhusu hatma ya wakimbizi wa Burundi

Pakua

Takriban raia wa Burundi 100,000 wamekimbilia Tanzania, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo tangu machafuko yaibuke mwishoni mwa mwezi Aprili. UNHCR, nchi zinazowapa hifadhi na wadau kwenye ukanda, wanajitahidi kuwapa usaidizi na mahitaji yao ya kimsingi.

Wengi wa wanaokimbilia Tanzania wamewasili kwenye rasi ya Kagunga, kijiji kimoja kilichojitenga kwenye ufukwe wa Ziwa Tanganyika, ambako rasilmali ni adimu. Kutoka hapo, wanasafirishwa kwa feri hadi kwenye uwanja wa michezo wa Kigoma, ambako watapewa chakula, makazi, pamoja na maji safi na huduma za kujisafi.

Wakimbizi wanaoishi kwenye uwanja watahamishiwa kwenye kambi zilizo karibu baadaye. Ungana na Joshua Mmali, akisimulia kuhusu hatma ya wakimbizi hao katika Makala ifuatayo

Photo Credit
Wakimbizi wanaokimbilia Tanzania kutoka Burundi(Picha ya UM/UNifeed)