Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

UN Photo/Shareef Sarhan

Michezo kwa amani, maendeleo na furaha.

Michezo ikitumiwa vyema yaweza kuleta hamasa ya maendeleo na amani katika jamii licha ya faida nyinginezo ikiwamo mshikamano na afya kwa wale wanaojihusisha nayo.

Katika muktadha huo, hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, kumekuwa na tukio maalum juma hili la kuadhimisha siku ya michezo kwa amani na maendeleo ambapo wadau wa michezo na maendeleo wameeleza namna dhana hizo zinavyotegemeana.

Joseph Msami amefuatilia umuhimu wa michezo na burudani katika jamii na kuandaa makala ifuatayo.

Nuru yaangazia harakati za ukatili wa Kingono, DRC kuna mafanikio

Ukatili wa kingono umekuwa tishio la maendeleo na ustawi wa wanawake na watoto hususan kwenye maeneo ya vita. Vikosi vya usalama na vile vilivyojihami hudaiwa kufanya vitendo hivyo ili kujenga hofu miongoni mwa jamii bila kujali kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Ni kwa kutambua hilo Baraza la usalama wiki hii limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu ukatili wa kingono hususan maeneo ya mizozo ambapo maeneo ya Kaskazini mashariki mwa Nigeria yaliangaziwa. Je nini kiliwekwa bayana? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.

UN Photo/Evan Schneider

Serikali mtuelewe Daadab isifungwe: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema tangazo la serikali ya Kenya kutoa muda wa miezi mitatu kuifunga kambi ya wakimbizi Daadab na kisha kuwarudisha makwao wakimbizi wa Somalia zaidi ya 350,000 limewastua , na kuitolea mwito serikali ya Kenya kutafakari upya.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii msemaji wa UNHCR nchini Kenya Emmanuel Nyabera amesema UNHCR imeanza mazungumzo na serikali ya Kenya ili kuangalia maeneo yanaoyoweza kufanyiwa kazi huku akikisistiza kuwa shirika hilo linatambua changamoto ya usalama inayolikumba taifa hilio kwa sasa.

Mataifa yawekeze katika sekta nyingine licha ya ugunduzi wa mafuta na gesi:UNCTAD

Ni lazima mataifa hususan yanayoendelea yawekeze katika sekta mbali mbali badala ya mafuta pekee ili kuweza kukabiliana na athari za kushuka kwa bei za mafuta hususan wakati huu ambao kunashuhudiwa kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo duniani. Hiyo ni sehemu ya ushauri aliotoaKatibu Mkuu wa Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD Mukhisa Kituyi alipohojiwa na Grace Kaneiya wa Idhaa kuhusu kongamano la bidhaa za kimataifa linaloendelea Geneva, Uswisi ambapo suala la bei ya mafuta na athari zake katika uchumi limepatiwa kipaumbele.

Elimu zaidi kuhusu asasi za kiraia na mchango wake yahitajika: Mlay

Vuguvugu la nafasi ya asasi za kiraia katika maendeleo hususan namna bora ya matumizi ya  rasilimali fedha linachukua kasi kimataifa amesema mmoja wa washiriki wa mkutano kuhusu uwezeshaji wa kifedha unaoendelea katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii Bi. Jovita Mlay ambaye anawakilisha mtandao wa wanawake wa Afrika katika sera za kiuchumi, AWEPON anasema kuelekea mkutano wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo nchini Ethiopia hamasa inahitajika zaidi. Kwanza anajibu swali nini ujumbe wa asasi anayoiwakilisha

Uganda yapambana na umasikini kupitia kilimo

Licha ya changamoto nyingi zikiwamo uitikio wa wananchi katika vita dhidi ya umaskini na baadhi ya wahudumu wa umma kujilimbikizia mali za kufadhili vita dhidi ya umaskini, Uganda inaendelea kupambana na umaskini.

John Kibego ameandaa makala kuhusu operesheni dhidi ya umaskini ambayo inaratibiwa na Jeshi la nchi hiyo baada ya kutovuna matunda mikononi mwa wahudumu wa umma kwa karibi muongo mmoja na nusu uliopita, ungana naye.

(MAKALA YA JOHN KIBEGO)

Mwakilishi wa Rwanda asema ni lazima kupambana na fikra za mauaji ya kimbari

Leo ikiwa ni miaka 21 baada ya kuanza kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Umoja wa Mataifa pamoja na Ujumbe wa Kudumu wa Rwanda kwenye Umoja huo wameandaa kumbukizi maalum jijini New York, kwa ajili ya kukumbuka mateso dhidi ya watutsi na baadhi ya wahutu walioyoyapitia nchini Rwanda mwaka 1994.

Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa, Jeanne d’Arc Byaje, ameeleza kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Ajira zisizo rasmi ni mtaji wa kiuchumi: Kabaka

Kurasimisha ajira zisizo rasmi mathalani vijana wanaotembeza bidhaa mikononi kwaweza kukuza sekta ya ajira,  hiyo ni kauli ya waziri wa kazi na ajira wa Tanzania, Gudencia Kabaka katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii mjini New York.

Waziri Kabaka ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano kuhusu mikakati mipya ili kufikia maendeleo endelevu pamoja na kutokomeza ukosefu wa ajira uliomalizika mjini New York ukiandaliwa na Baraza la Uchumi na la Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC na Shirika la Kazi Duniani ILO.