Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajira zisizo rasmi ni mtaji wa kiuchumi: Kabaka

Ajira zisizo rasmi ni mtaji wa kiuchumi: Kabaka

Pakua

Kurasimisha ajira zisizo rasmi mathalani vijana wanaotembeza bidhaa mikononi kwaweza kukuza sekta ya ajira,  hiyo ni kauli ya waziri wa kazi na ajira wa Tanzania, Gudencia Kabaka katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii mjini New York.

Waziri Kabaka ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano kuhusu mikakati mipya ili kufikia maendeleo endelevu pamoja na kutokomeza ukosefu wa ajira uliomalizika mjini New York ukiandaliwa na Baraza la Uchumi na la Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC na Shirika la Kazi Duniani ILO.

Kwanza Waziri huyu wa kazi wa Tanzania anaanza kwa kueleza dhana ya mkutano.

Photo Credit
Mama mfanyabiashara (Picha ya © Aude Rossignol / UNDP Burundi)