17 Oktoba 2022
Karibu kusikiliza jarida, Flora Nducha anakuletea yale yaliyojiri kutoka Umoja wa Mataifa ikiwemo;-
1. Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga umasikini ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema lazima hatua za dharura zichukuliwe, tena kwa kuzingatia watu na utu.
2. Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya watoto UNICEF nchini Uganda kwakushirikiana na serikali ya Japan wanaisaidia serikali ya Uganda kuimarisha mifumo ya afya ili watoto wote waweze kupata chanjo.