Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

02 Decemba 2021

Karibu kusikiliza Jarida miongoni mwa utakayosikia ni pamoja na 

- WFP watoa picha na video kuonesha hali inayoendelea nchini Afghanistan na kuomba jumuiya za kimataifa kutenganisha siasa na misaada ya kibinadamu ili wawasaidia wananchi wanaoteseka.

- Wananchi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati wamewashukuru mapolisi wa Umoja wa Mataifa

- UNHCR ina wasiwasi na hali ya wakimbizi wa ndani ambao ni watu wa asili Waruo huko Guyana nchini Venezuela 

pia utapata kusikia Makala kutoka Uganda na mashinani walichosema wanawake wa Burkina Faso

Sauti
14'8"

01 Desemba 2021

Leo ni siku ya UKIMWI duniani karibu tuwe sote katika mada kwa kina ambayo inatupeleka makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na Utamaduni UNESCO mjini Paris Ufaransa kuangazia mchakato wa kupitisha azimio la kuwa na siku ya Kiswahili duniani, Utasikia Azimio hilo linamaanisha nini? Na je baada ya kutengwa siku ya Kiswahili nini kinafuata?. Ungana na Flora Nducha aliyefanya mahojiano maalum na Balozi wa Tanzania huko Ufaransa Samwel Shelukindo 

Sauti
12'46"