Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 Oktoba 2020

30 Oktoba 2020

Pakua

Katika kuelekea siku ya miji duniani hapo kesho Oktoba 31, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Abtonio Guterres kupitia ujumbe maalum wa siku hiyo amesema miji imebeba gharama kubwa ya janga la corona au COVID-19 lakini jamii katika miji hiyo zimedhihirisha thamani yake katika kukabiliana nalo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP kwa kushirikiana na serikali ya Kenya leo wamezindua mpango wa ugawaji fedha taslim kwa familia 24,000 mjini Mombasa  katika makazi yasiyo rasmi ambao Maisha yao yamesambaratishwa na athari za janga la COVID-19.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amesisitiza umuhimu wa kuwawezesha wanawake nchini Colombia ili kuendelea kuchagiza mchakato wa amani nchini humo.

Pia tunamsilikiza kijana ambaye amekamilisha mafunzo kwa vitendo katika Idara ya habari na mawasiliano na Umoja wa Mataifa kupitia Idhaa hii ya Kiswahili ambayo ndiyo hukuletea jarida hili na habari nyingine za UN kupitia redio na televisheni washirika pamoja na wavuti wa news.un.org/sw/. 

Audio Credit
Flora Nducha
Sauti
10'48"