Mradi uliofadhiliwa na TAKEDA, wawezesha Rwanda kuimarisha huduma kwenye hospitali na vituo vya afya: UNICEF
Nchini Rwanda, Umoja wa Mataifa unashirikiana na serikali kuimairisha huduma za uzazi ili hatimaye kuhakikisha kila uzazi unakuwa salama si tu kwa mama bali pia mtoto anayezaliwa. Kupitia mradi uliofadhiliwa na TAKEDA, kampuni hii ya utafiti na dawa duniani, Rwanda imeweza kuimarisha huduma kwenye hospitali na vituo vya afya.
Mradi huo wa ubia ulianza mwaka 2017. Wakati huo, Rwanda ndio ilikuwa imekamilisha malengo ya milenia, ikimaanisha baadhi ya malengo yalitimizwa, lakini kulikuwa na kusuasua katika baadhi ya maeneo mengine.