Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP na GEP kwa kufanikisha mlo shuleni Burundi tayari inaonesha matokeo – UNICEF

WFP na GEP kwa kufanikisha mlo shuleni Burundi tayari inaonesha matokeo – UNICEF

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linaripoti kuwa huduma ya chakula katika baadhi ya shule za msingi nchini Burundi tayari inaonesha matokeo chanya kuanzia mahudhurio shuleni na katika upande wa taaluma.

Burundi, nchi yenye udongo mzuri wenye rutuba ambayo kama si mabadiliko ya tabianchi kuathiri baadhi ya maeneo, changamoto ya kukosekana kwa chakula ingekuwa simulizi tu za kufikirika.

Lakini kama anavyoeleza Leandre Nkuzimana ambaye ni Mkurugenzi wa elimu katika eneo la Kirundo ni kuwa mabadiliko ya tabianchi ni kitu halisi na mfano halisi ni athari kwa mavuno ya eneo la Kirundo na hivyo kufanya wakati mwingine watoto kutoenda shule na wengine wakienda kufanya kazi za vibarua katika maeneo mengine ya mbali yenye mavuno.

UNICEF inatoa shukrani kwa msaada wa Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya Elimu (GEP) kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP) wamefanikisha mlo katika baadhi ya shule nchini Burundi na watoto zaidi ya elfu thelathini katika shule takribani 40 wamefaidika na mradi huu wa mlo shuleni.

Fabrice Ntirandekura ni mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya msingi Kibonde ni shuhuda, “Tunapata chakula katika kantini ya shule. Hii inatufanya tuwe na ari ya kwenda shule kwa sababu bila chakula wanafunzi wengi wanaacha shule na wanasalia watoto wachache sana.”

Audio Credit
Edouige Emerusenge
Sauti
1'45"
Photo Credit
WFP/Hugh Rutherford