Mkuu wa UNHCR ajionea hali halisi ya wakimbizi wa ndani huko Tigray Ethiopia
Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Fillipo Grandi ametembelea kambi ya wakimbizi ya Mai-Aini katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia, na kujionea hali ilivyo na akaiahidi serikali kusaidia kupunguza madhara ya hali hiyo kwa raia. Taarifa ya Ahimidiwe Olotu inaeleza zaidi.