Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UN

Tusimamie maadili ya Mandela na kuziba pengo la usawa, tukimuenzi: UN

Katika kuelekea siku ya kimataifa ya Nelson Mandela hapo Jumamosi Julai 18, siku ya kuzaliwa kwa mwanaharakati huyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni muhimu kumuenzi kwa kupigania maadili yake kama kuziba pengo la usawa. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

Kupitia ujumbe wake wa siku hiyo ya Mandela , Guterres amesema ni ya kutoa heshima kwake kama mtetezi wa ulimwengu wenye usawa, utu na mshikamano.

Sauti
3'36"
MONUSCO/Force

FIB ya MONUSCO yachukua hatua kuimarisha ulinzi Matembo na Ngadi, DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB, cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, kimefikia makubaliano na wakazi wa kata za Ngadi na  Matembo jimboni Kivu Kaskazini ya kutekeleza mradi wa taa za barabarani kama njia mojawapo ya kuimarisha usalama kwenye eneo hilo lililogubikwa na vikundi vilivyojihami vinavyoshambulia raia. Issa Mwakalambo, wa kikundi cha 7 cha Tanzania, TANZBATT 7 na maelezo zaidi.

Sauti
3'11"
Picha/UN-Habitat/Julius Mwelu

Kuwa kinyozi ni talanta yangu:Mkimbizi Tekla

Kutana na mkimbizi Tekla kutoka Eritrea ambaye umri wake ni miaka 15, safari ya kwenda kusaka maisha Ulaya iliishia mahabusu Libya na baada ya kuokolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR hivi sasa ni kinyozi mashuhuri kwenye kambi ya muda ya Hamdallaye  nje ya mji mkuu Niamey nchini Niger. Jason Nyakundi anasimulia zaidi

Sauti
2'8"
UN-Habitat/Julius Mwelu

Nchini Tanzania, UNCDF yachochea maendeleo mji wa Kibaha

Mtaji kutoka shirika la maendeleo ya mitaji la Umoja wa Mataifa, UNCDF kwa halmashauri ya mji wa Kibaha mkoani Pwani nchini Tanzania umewezesha ujenzi wa kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani na hivyo kuchochea maendeleo si tu ya jamii bali ya mkoa husika. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

UNCDF ilifanya kazi na halmashauri ya mji wa Kibaha kwa kuipatia mtaij wa fedha wa uwekezaji na msaada wa kiufundi katika kujenga kituo kipya cha basi.

Sauti
2'34"
UNIC Dar es Salaam/Ahimidiwe Olotu

Sasa ndoto za watoto kuwa marubani Tanzania zaanza kutimia

Nchini Tanzania, taasisi ya kijamii ya Tanzania Youth Aviation, yenye lengo la kuhamasisha vijana na watoto kuingia katika faniya urubani na uongozaji wa ndege imeanza kufanikiwa katika kufikia lengo lake hilo wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa na wadau wanataka wasichana nao wajiunge na masomo ya sayansi, teknolojia  na hisabati, STEM. Ahimidiwe Olotu na maelezo zaidi.

Sauti
2'4"