Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwa kinyozi ni talanta yangu:Mkimbizi Tekla

Kuwa kinyozi ni talanta yangu:Mkimbizi Tekla

Pakua

Kutana na mkimbizi Tekla kutoka Eritrea ambaye umri wake ni miaka 15, safari ya kwenda kusaka maisha Ulaya iliishia mahabusu Libya na baada ya kuokolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR hivi sasa ni kinyozi mashuhuri kwenye kambi ya muda ya Hamdallaye  nje ya mji mkuu Niamey nchini Niger. Jason Nyakundi anasimulia zaidi

Tekla ambaye ni maarufu kambini hapo kwa kazi nzuri ya kunyoa nywele katika mitindo mbalimbali akinadi moja ya mitindo katika kichwa chake na kwamba ni kazi anayoipa umuhimu mkubwa.Aliondoka Eritrea akiwa na umri wa miaka 13 tu kwa lengo la kwenda Ulaya miaka miwili iliyopita na alipofika Libya akijikuta katika vituo vya kushikilia wakimbizi kwa miaka miwli baada ya kujaribu kupanda boti kwenda Ulaya na kurejeshwa Tripoli na mamlaka ya Libya.

Tekla miongoni mwa watoto 500 wasio na wazazi au walezi waliokolewa na UNHCR kutoka kwenye vituo vya kushikilia wakimbizi Libya na kupelekwa Niger ambako wanapatiwa msaada wa huduma za msingi ikiwemo malazi na chakula wakisubiri kupelekwa nchi ya tatu.

Kupitia mafunzo yanayotolewa na UNHCR kambini hapo Tekla amegeuza talanta yake ya kunyoa kuwa kazi inayompatia kipato na anasema wengi wa wateja wake humtaka awachagulie mitindo ya kukata nywele "Hii ndio kazi pekee ninayojua kufanya, hapo mwanzo sikuwa na mashine inayotumia umeme nilikuwa natumia mkasi na wembe.”Tekla sasa ana vifaa vyote vinavyohitajika .

Talanta yake ilianzia kwa kukata nywele za rafiki zake nyumbani Eritrea na sasa katika kambi hii yeye na watoto wengine zaidi 160 wanapatiwa mafunzo ya stadi za maisha wakiwemo 15 wanaojifunza kuwa vinyozi. Aboubacar Niandou ni mmoja wa waendesha mafunzo“Ninawafundisha wakimbizi kukata nywele, wanaipenda sana kazi hiyo, ni kazi nzuri yenye faida nyingi.”Ingawa vijana hawa akiwemo Tekla waliporwa haki ya kupata elimu UNHCR na wadau wengine wa misaada wanawapa fursa ya kujitegemea kwa kuwafunza stadi mbalimbali pamoja na lugha na wengi wao watapata maskani mapya katika nchi ya tatu baada ya mwaka mmoja.

Audio Credit
Flora Nducha/Jason Nyakundi
Audio Duration
2'8"
Photo Credit
Picha/UN-Habitat/Julius Mwelu