Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Tuchukue hatua Mediteranea irejee katika hali yake ya awali- Guterres

Fursa za kiuchumi na kijamii kwenye ukanda wa Mediteranea ambao kihistoria unatambulika kwa maendeleo ya kitamaduni, hivi sasa ziko mashakani kutokana na ukanda huo kughubikwa na matatizo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema hayo akihutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichokutana leo kujadili changamoto za amani na usalama kwenye ukanda huo unaojumuisha nchi zote zinazozingira bahari ya Mediteranea.

Msafiri Zawose aendelea kupigia chepuo muziki wa asili Tanzania

Muziki wa asili umekuwa haupatiwi kipaumbele na vijana wengi maeneo mbali mbali duniani licha ya kuwa ni sehemu ya utamaduni wao kwani unazungumzia asili yao. Lakini hali ni tofauti kwa mwanamuziki wa muziki wa asili kutoka nchini Tanzania  Msafiri Zawose ambaye licha ya vijana wenzake wengi kujikita katika muziki wa kizazi kipya almaarufu  bongo fleva yeye ameamua kuitangaza nchi yake kupitia muziki asilia. Je anafanya nini? Namkeshe Msangi wa Radio washirika Voice of Afrika kutoka Korogwe Tanzania amezungumza naye katika makala hii ya midundo.

Tuna wasiwasi na cambodia baada ya chama cha upinzani kufutwa: Zeid

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein ameonyesha hali  ya wasiwasi  juu ya kuwepo kwa uwazi na uhuru kwenye uchaguzi nchini Cambodia baada ya mahakama kuu nchini  humo  kufuta usajili wa chama kikuu cha upinzani kwa miaka mitano.

Chama hicho, CNRP ambacho ni kikuu cha upinzani Cambodia kimekuwa kinapinga uamuzi wa mahakama kuzuia uhuru wa vyombo vya habari nchi humo huku wizara ya mambo ya ndani ikidai kuaw kimekuwa kikipanga  njama za mapinduzi dhidi ya serikali.

Nishati ya jua yaleta ahueni kwa warohingya Cox’s Bazar- IOM

Nishati ya jua imeleta nafuu katika utoaji wa huduma za afya kwenye wilaya ya Cox’s Bazar nchini Bangladesh ambako mamia ya maelfu ya wakimbizi warohingya kutoka Myanmar wamesaka hifadhi.

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM limesema wamechukua hatua hiyo ili kuweza kutoa huduma mchana na usiku kutokana na ongezeko kubwa la watu wanaohitaji huduma za afya.

Tangu mwezi Agosti mwaka huu zaidi ya warohingya waliosaka hifadhi eneo hilo ni zaidi ya laki 8 ambapo wanakabiliwa na matatizo ya kiafya.

Joel Millman ni msemaji wa IOM, Geneva Uswisi.

Warohingya sasa watumia vyelezo kukimbia Myanmar- UNHCR

Harakati za warohingya kukimbia nchi yao Myanmar kutokana na mateso zinazidi kutia wasiwasi zaidi wakati huu ambapo wanaendelea kumiminika Bangladesh kwa kutumia usafiri unaotishia zaidi maisha yao.

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema hivi sasa warohingya wanatumia vyelezo walivyojitengenezea wenyewe kwa kutumia mianzi na makopo na hivyo kuhatarisha maisha yao majini.

Dola Millioni 100 zahitajika kuokoa watu kutokana na majanga

Shirika la umoja wa Mataifa la hali ya hewa WMO, linataka hatua zaidi zichukuliwe ili kufanikisha mfuko wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na pia kutoa taarifa mapema uitwao CREWS.

Mfuko huo unahitaji dola milioni 100 ifikapo mwaka 2020 ambapo WMO inataka kasi zaidi ya uchangiaji ili kusaidia nchi maskini zilizo katika hatari za kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.

WMO imesema bila uwekezaji pia katika mfuko huo msaada kwa nchi maskini kukabili mabadiliko ya tabianchi itakuwa matatizo makubwa.

Tunapopambana na ugaidi lazima tuheshimu haki za binadamu: Guterres

Haki za binadamu bila shaka ni shememu kubwa ya suluhu ya vita dhidi ya ugaidi, amesema leo mjini London Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika hotuba yake kwenye chuo kikuu cha masomo ya Mashariki na Afrika SOAS.

Ameongeza kuwa"Ugaidi unashamiri wakati watu wasiokuwa na wasiwasi wanapokutana na mitazamo tofauti na kupoteza imani na mara nyingi miziz yake ni kutokuwa na matumaini na kukata tamaa na ndio sababu, haki zote za binadamu zikiwemo za kiuchumi, kijamii na kitamaduni bila shaka ni sehemu ya suluhu katika vita dhidi ya ugaidi kwani