Tuna wasiwasi na cambodia baada ya chama cha upinzani kufutwa: Zeid
Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein ameonyesha hali ya wasiwasi juu ya kuwepo kwa uwazi na uhuru kwenye uchaguzi nchini Cambodia baada ya mahakama kuu nchini humo kufuta usajili wa chama kikuu cha upinzani kwa miaka mitano.
Chama hicho, CNRP ambacho ni kikuu cha upinzani Cambodia kimekuwa kinapinga uamuzi wa mahakama kuzuia uhuru wa vyombo vya habari nchi humo huku wizara ya mambo ya ndani ikidai kuaw kimekuwa kikipanga njama za mapinduzi dhidi ya serikali.
Bwana Zeid amesema demokrasia yenye ufanisi inahitaji upinzani ambao unaweza kufanya kazi kwa uhuru bila vitisho , ameongeza kuwa matukio hayo yote ni kiashirio cha ukiukwaji wa haki za binadamu, na pia ukiukwazi wa haki za kukusanyiko kwa mujibu wa sheria ya kimataifa.
Ikumbukwe kuwa rais wa chama hicho cha CNRP Kem Sokha alifungwa mnamo tarehe 3 Septemba wa mwaka 2013 kwa mashtaka ya uasi .