Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Warohingya sasa watumia vyelezo kukimbia Myanmar- UNHCR

Warohingya sasa watumia vyelezo kukimbia Myanmar- UNHCR

Pakua

Harakati za warohingya kukimbia nchi yao Myanmar kutokana na mateso zinazidi kutia wasiwasi zaidi wakati huu ambapo wanaendelea kumiminika Bangladesh kwa kutumia usafiri unaotishia zaidi maisha yao.

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema hivi sasa warohingya wanatumia vyelezo walivyojitengenezea wenyewe kwa kutumia mianzi na makopo na hivyo kuhatarisha maisha yao majini.

Msemaji wa UNHCR huko Geneva, Uswisi, William Splinder amesema wamepokea ripoti kuwa katika siku 10 zilizopita, takribani vyelezo 30 vimewasili kutoka Myanmar vikiwa vimebeba warohingya.

Amesema safari ya saa nne kwa kutumia vyelezo ni hatari wakati huu  imeelezwa kuwa hadi sasa warohingya zaidi ya 100 wamekufa maji tangu mzozo huo uanze tarehe 25 mwezi Agosti.

Photo Credit
Warohingya watumia vyelezo kukimbia Myanmar. © UNHCR/Andrew McConnell