Neema ya maji safi kwa wanavijiji wa Buliisa nchini Uganda
Pakua
Suala la maji safi na salama ni moja ya mambo muhimu katika ajenda ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs yenye ukomo wake mwaka 2030. Katika kufuatilia utekelezaji wa ajenda hiyo, mwandishi wetu nchini Uganda John kibego amepata fursa ya kutembelea wilaya ya Buliisa karibu na ziwa Albert nchini humo ambapo amezungumza na wenyeji kufuatia tatizo la maji salama wanalokabiliana nao .
Ukosefu wa maji salama katika wilaya ya Buliza umeathiri maisha ya baadhi ya wanavijiji kutokana na magonjwa kama vile kipindupindu na baadhi yao kupoteza maisha kutokana na matumizi ya maji yasiosalama .
Hata hivyo habari njema kwa wanavijiji katika eneo la ziwa Albert ni kwamba serikali ya Uganda kwa msaada wa mashirika ya kimataifa wamezindua mradi wa maji safi utakaosadidia na pia kuokoa maisha ya wengi kama anavyotuhabarisha John kibego katika makala hii.