Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Uhalifu dhidi ya wahamiaji Libya unaweza kuwajibishwa kupitia ICC

Uhalifu dhidi ya wahamiaji waliofungwa au kusafirishwa kwa njia haramu kupitia Libya unaweza kuwajibishwa chini ya mamlaka ya  mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC.

Kauli hiyo imetolewa na mwendesha mashtaka wa ICC, Bi Fatou Bensouda, akihutubia kikao cha Baraza la Usalama kilichokutana leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kujadili hali nchini Libya.

Bi Bensouda amesema iwapo ukatili mkubwa unaendelea kutekelezwa , kwa kutumia mkataba wa Roma hata sita kutoa tangazo la kukamatwa kwa wahalifu wanaotekeleza vitendo hiyvo.

Programu ya uanagenzi ya ILO yaleta nuru kwa vijana Tanzania

Shirika la Kazi Duniani ILO kwa kushirikiana na Serikali ya Norway wamesaidia vijana kwenye ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika kuboresha stadi zao katika biashara na pia kuwapa fursa za ajira katika sekta mbalimbali kama vile za hoteli na utalii. Hii ni sehemu ya uanagenzi wa kuhakikisha wanafunzi wanapata mafunzo ya kinadharia na vitendo ili wanapomaliza masomo yao wawe na stadi za kutosha. Je wamefanya nini? Selina Jerobon amefuatilia makala hii.

Brazil inatakiwa kuendeleza vita dhidi ya utumwa wa kisasa UM

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa  leo wametoa wito kwa serikali ya Brazil kuchukua hatua za haraka katika  mapambano  dhidi ya utumwa wa kisasa unaodhoofisha kanuni za ushirika.

Urmila Bhoola ambaye ni mtalaam huru wa haki za binadam wa Umoja wa Mataifa amesema, vitendo vya utumwa wa kisasa vinaongeza nchini humo na ni hali inayotia wasiwasi kufuatia maamuzi ya wizara kifungu namba 1129 kinachopunguza  kutilkia mkazo mapampano dhidi ya vitendo vya utumwa wa kisasa.

Urusi yageuza madeni ya Msumbiji kutoa mlo mashuleni:WFP

Mpango wa kubadili madeni kati ya Shirikisho la Urusi na serikali ya Msumbiji umeweka ahadi ya dola milioni 40 za Marekani, ambazo zitatumiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP) ili kusaidia Serikali ya Msumbiji kutoa mlo mashuleni  kwa watoto 150,000 nchini humo kwa zaidi ya miaka mitano ijayo.

Mbali na kufuta madeni kwa Msumbiji, mpango huo utatoa rasilimali mpya kwa ajili ya maendeleo na kusaidia upanuzi wa mpango wa kitaifa wa mlo shuleni ambao unalenga kutoa chakula katika shule zote za msingi nchini Msumbiji.

Kijitabu chazinduliwa kuimarisha afya kwenye sekta ya kilimo cha ndizi

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kwa kushirikiana na serikali  ya Ecuador leo wamezindua kijitabu cha maelekezo chenye lengo la kuboresha mazingira ya kazi na afya ya wafanyakazi wanaozalisha ndizi.

FAO kupitia taarifa yake inasema mahitaji ya ndizi ni makubwa duniani na kutokana na hali hiyo wamiliki wa sekta hiyo hutumia kila mbinu kupunguza gharama za uzalishaji hali ambayo ina madhara makubwa kwa haki za wafanyakazi na mazingira.

Acheni kutumia viuavijasumu ili kuzuia usugu wa dawa:WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO linapendekeza wakulima na sekta ya chakula kuacha matumizi ya viuavijasumu au antibiotics mara kwa mara ili kukuza haraka mifugo na kuzuia magonjwa kwa wanyama wenye afya.

Mapendekezo hayo mapya ya WHO yaliyotolewa leo yanalenga kusaidia kulinda uwezo wa dawa za viuavijasumu ambazo ni muhimu kwa matumizi ya binadamu kwa kupungua matumizi yasiyohitajika ya dawa hizo kwa wanyama.