Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kijitabu chazinduliwa kuimarisha afya kwenye sekta ya kilimo cha ndizi

Kijitabu chazinduliwa kuimarisha afya kwenye sekta ya kilimo cha ndizi

Pakua

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kwa kushirikiana na serikali  ya Ecuador leo wamezindua kijitabu cha maelekezo chenye lengo la kuboresha mazingira ya kazi na afya ya wafanyakazi wanaozalisha ndizi.

FAO kupitia taarifa yake inasema mahitaji ya ndizi ni makubwa duniani na kutokana na hali hiyo wamiliki wa sekta hiyo hutumia kila mbinu kupunguza gharama za uzalishaji hali ambayo ina madhara makubwa kwa haki za wafanyakazi na mazingira.

Uzinduzi huo umefanyika Geneva, Uswisi ambapo kijitabu hicho kina mapendekezo lukuki mathalani matumizi salama ya dawa za kuua vijidudu kwenye mazao, kuepusha ukatili wa kijinsia na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kupitia mwongozo huo wafanyakazi na wakufunzi watatambua jinsi ya kukabiliana na hatari kwenye kilimo cha migomba na kufanya kazi kwa usalama zaidi.

Uzalishaji wa ndizi kupitia kilimo cha migomba ni muhimu kama chanzo cha ajira na kipato kwa maelfu ya kaya za vijijini kwenye nchi zinazoendelea.

Ecuador ndio inaongoza duniani kwa kuzalisha kiasi kikubwa cha ndizi ambazo hutumika kama tunda lakini vile vile hupikwa kama chakula.

Photo Credit
Wakulima wa ndizi. Picha: FAO