Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Acheni kutumia viuavijasumu ili kuzuia usugu wa dawa:WHO

Acheni kutumia viuavijasumu ili kuzuia usugu wa dawa:WHO

Pakua

Shirika la afya ulimwenguni WHO linapendekeza wakulima na sekta ya chakula kuacha matumizi ya viuavijasumu au antibiotics mara kwa mara ili kukuza haraka mifugo na kuzuia magonjwa kwa wanyama wenye afya.

Mapendekezo hayo mapya ya WHO yaliyotolewa leo yanalenga kusaidia kulinda uwezo wa dawa za viuavijasumu ambazo ni muhimu kwa matumizi ya binadamu kwa kupungua matumizi yasiyohitajika ya dawa hizo kwa wanyama.

Kwa mujibu wa muongozo huo katika baadhi ya nchi takribani asilimia 80 ya matumizi ya dawa hizo muhimu za viuavijasumu yanafanyika kwenye sekta ya mifugo na kwa sehemu kubwa ni kusadia kukuza haraka mifugo hiyo ambayo haina maradhi yoyote.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus amesisitiza kwamba matumizi mbaya ya dawa hizo na matumiazi ya kupindukia kwa mifugo na binadamu yanasababisha usugu wa dawa ambao athari na gharama zake zitakuwa kubwa sana hasa kwa binadamu lakini pia ni tishio kwa usalama hasa kunapozuka magonjwa ya mlipuko ynayosababisha vifo na dawa hizo kushindwa kufanya kazi..

Photo Credit
Kuku, WHO linasema wafugaji wasitumie Viua Vijasumu kwa mifugo wenye afya nzuri. Picha: WHO