Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauaji ya mfanyakazi wa Televishen ya Shamshad Afghanistan

UNESCO yalaani mauaji ya mfanyakazi wa Televishen ya Shamshad Afghanistan

Pakua

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova , leo amelaani vikali mauaji ya mfanyakazi wa televisheni ya Shamshad, yaliyotokea jana mjini Kabul  Afghanistan baada ya mtu mwenye silaha kuvamia ofisi za televisheni hiyo na kujeruhi pia wafanyakazi wengine kadhaa.

Bokova ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mfanyakazi huyo aliyekuwa mlinzi wa kituo hicho cha televisheni, kuwatakia ahuweni ya haraka majeruhi na pia kuwapongeza kwa ujasiri wao wa kurejea hewani kwenye vipindi muda mfupi tu baada ya shambulio hilo la kigaidi.

Mtu mwenye silaha aliyevalia kama polisi alivamia ofisi za kituo cha televisheni cha Shamshad baada ya kumuua mlinzi wa kituo hicho getini wafanyakazi wengine zaidi ya 20 walijeruhiwa, huku sita kati yao wakielezwa kuwa kwenye hali mahtuti.

Televisheni ya Shamshad ni kituo binafsi kinachorusha matangazo ya elimu, habari na burudani kwa saa 24.

Photo Credit
UNESCO limesisitiza usalama wa waandishi wa habari. Picha: UNESCO