Tamasha la Kusini-Kusini 2017 lakunja jamvi Uturuki

Tamasha la Kusini-Kusini 2017 lakunja jamvi Uturuki

Pakua

Tamasha la kimataifa la ushirika wa Kusini-Kusini mwaka 2017 leo limekunja jamvi mjini Antalya Uturuki huku umoja wa Mataifa na wadau wakifurahia matokeo .

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa ofisi ya Umoja wa mataifa ya ushirika wa Kusini-kusini Jorge Chediek, lengo la tamasha hilo ambalo huandaliwa kila mwaka ni kutoa fursa kwa nchi za Kusini -Kusini , taasisi mbalimbali na mataifa mengine yakiwepo ya Kaskazini kujumuika pamoja na kuanzisha ushirika mpya ili kufaidika na ushirika wa Kusini-kusini na kwa mwaka huu amesema lengo limetia na kuongeza kuwa

(CHEDIEK CUT)

“Mafanikio mengi ya tamasha hili hayapo tu katika idadi kubwa ya washiriki, bali yapo katika ushirika ambao umeanzishwa katika urafiki wa taasisi na makubaliano yaliyoanzishwa ambayo bila shaka yatazaa matunda.”

Tamasha la mwaka huu liliwateta pamoja washiriki zaidi ya 800 kutoka nchi 120 wakiwemo wawakilishi zaidi ya 30 wa vyombo vya habari, huku maelfu mengine ya watu walishiriki kupitia vyombo vya habari na mitandao.

Umoja wa Mataifa umeishukuru serikali ya Uturuki kuwa mwenyeji wa tamasha hilo na kudumisha ushirika wa muda mrefu kati yao.

TAGS:

Photo Credit
Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Ushirikiano wa Kusini Kusini Jorge Chediek akitoa hotuba katika mkutano wa Expo ya Kusini Kusini ya Maendeleo Expo huko Antalya, Uturuki. DPI / Maoqi Li