Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marufuku ya "viroba" Tanzania yaleta nuru kwa vijana

Marufuku ya "viroba" Tanzania yaleta nuru kwa vijana

Pakua

Katika ajenda ya Umoja  wa Mataifa ya  malengo ya  maendeleo endelevu SDGs au ajenda  2030, vijana kama nguvu kazi na mustakabali wa dunia wanapewa jukumu la kijiendeleza ili kujikwamua na suala la umasikini siku za usoni.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika hutuba yake huko Abidjan, Cote D’Ivoire amezieleza  serikali  za Afrika na zile za Ulaya  kwamba ili kufikia  mustakhbali bora ni lazima kuwekeza katika vijana leo.

Katika kufanikisha hilo, Alex Punte wa radio washirika, Kyela FM huko Mbeya nchini Tanzania anatupeleka Kyela mjini ambako kuna nuru sasa kwa vijana baada ya serikali ya Tanzania kupiga marufuku matumizi ya pombe zilizokuwa zinauzwa kwenye vifungashio vya vifuko, maarufu kama viroba, ambayo ilikuwa inaathiri sana vijana na hivyo kuhatarisha mustakhbali wao.

Photo Credit
Marufuku ya "viroba" Tanzania yaleta nuru kwa vijana. Picha: UM