Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa kifua kikuu, changamoto na tiba

Ugonjwa wa kifua kikuu, changamoto na tiba

Pakua

Kifua kikuu au TB!Gonjwa lililoorodheshwa na shirika la afya ulimwengni WHO kuwa miongoni mwa magonjwa 10 yanayoongoza kwa kusababisha vifo duniani.

WHO inasema mathalani mwaka 2015 watu milioni 10.4 waliugua ugonjwa huo, milioni 1.8 walifariki duniani, wakiwemo takribari watu Laki tano ambao walikuwa na virusi vya Ukimwi, VVU. Miongoni mwa waathirika ni kundi la wahamiaji ambalo katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani tarehe 24 mwezi Machi, limeangaziwa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM linasema jamii zilizo hatarini kama vile wahamiaji na wakimbizi zinapaswa kufikiwa kwa kuelimishwa kwani ugonjwa huo husababisha unyanyapaa na ubaguzi na hivyo kupunguza fursa hususani za matibabu kwa wahamiaji. Uganda ni miongoni mwa nchi zinazohifadhi wahamiaji ambako mwandishi wetu  Johh Kibego amewatembelea kufahamu majaliwa yao dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu.

Photo Credit
TB ni ugonjwa ambao unaambukiza na kinga ni muhimu.(Picha:UNifeed/video capture)