Skip to main content

Uganda iko tayari kuongeza kasi ya vita dhidi ya Ukimwi

Uganda iko tayari kuongeza kasi ya vita dhidi ya Ukimwi

Pakua

Mkurugenzi wa timu ya kanda ya Mashariki na kusini mwa Afrika wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS, Bi Sheila Tlou, amezuru Uganda ili kuchagiza hatua za kushughulikia mwenendo wa ongezeko la maambukizi mapya ya ukimwi nchini humo.

Kwa mujibu wa takwimu za UNAIDS, kuna maambukizi mapya 360 kila wiki Uganda miongoni mwa wasichana vigori na wanawake wenye umri wa kati ya miaka 15-24.

Uganda imetajwa kama moja ya nchi ambazo zinaweza kuleta mabadiliko ya kasi duniani ambayo yatachangia kukomesha ukimwi kama tishio la afya ya umma ifikapo 2030.

Bi Tlou amempongeza mke wa Rais wa Uganda Bi,Janet Museveni,kwa juhudi za taifa hilo kuzuia maambukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ambapo Uganda imeshuhudia kushuka kwa asilimia 86 maambukizi kwa watoto kutoka mwaka 2009 hadi 2015.

Photo Credit
Janeth Museveni (kushoto) na Sheila Tlou. Picha: UNAIDS Uganda