Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maandishi 11 mapya yaongezwa kwenye orodha ya turathi za tamaduni: UNESCO

Maandishi 11 mapya yaongezwa kwenye orodha ya turathi za tamaduni: UNESCO

Pakua

Maandishi mapya 11 leo yameongezwa kwenye orodha ya turathi za tamaduni zisizogusika za Kibinadamu za shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamasduni UNESCO.

Uamuzi huo umefikiwa leo mjini Addis Ababa Ethiopia kwenye mkutano ulioandaliwa na serikali na UNESCO utakaomalizika Desemba pili. Maandishi hayo yamekidhi vigezo ikiwa ni pamoja na ufahamu wa umuhimu wake katika jamii.

Miongoni mwa maandishi hayo ni mfumo wa Gada nchini Ethiopia ambao ni mfumo wa kiasili wa utawala kwa watu wa kabila la Oromo ulioanzishwa kutokana na elimu ya kurithishana kutoa vizazi hadi vizazi. Mfumo huo unafunzwa kwa njia ya simulizi na wanahistoria.

Photo Credit
Picha: UNESCO Logo