Kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Uhuru wa kujieleza ni moja ya haki muhimu kwa watu, na ni uhuru unaozidi uhuru wa aina yoyote ile na kutoa msingi wa utu wa mtu.
Uhuru wa kujieleza ni moja ya haki muhimu kwa watu, na ni uhuru unaozidi uhuru wa aina yoyote ile na kutoa msingi wa utu wa mtu.
Wakati ulimwengu umeadhimisha siku ya Malaria bado nchi hasa zilizo maskini hazijapata suluhu kamili na njia mwafaka za kupambana na kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.
Caroline Khamati Mugalla ni afisa kutoka shirika la muungano wa wafanyakazi Afrika Mashariki amehudhuria mkutano wa UNCTAD unaoendelea nchini Qatar, Doha. Amepata kuzungumza na afisa kutoka redio ya Umoja wa Mataifa na alikuwa na haya ya kusema...
(MAHOJIANO YA CAROLINE MUGALLA)
Umoja wa Mataifa, ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na wanaharakati mbalimbali wa kupigania haki ikiwa ni pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali wameendelea kupaza sauti wakizitaka serikali duniani kutambua na kuheshimu haki za wanawake na wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja
Leo ni siku ya afya duniani, Umoja wa Mataifa waungana na dunia kuadhimisha siku hii ambayo kwa mwaka huu inajikita kupiga darubini masuala ya afya na uzee.
Shirika la wahamiaji la IOM limesema msafara wa magari yanayosafirisha raia wa Sudan Kusini wanaorejea nyumbani kutoka Sudan Kaskazini umekwama katikati ya mapigano kati ya waasi na majeshi ya Sudan Kusini.
Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya maji ambayo kauli mbiu ya mwaka huu ni "maji na usalama wa chakula" inaonekana kuwa nchi nyingi zimepiga hatua katika udhibiti wa maji lakini bado juhudi zaidi zinahitajika.
Takribani watu milioni 5 wenye umri wa miaka 30 na zaidi wamekufa kutokana na matumizi ya moja kwa moja ya tumbaku kote duniani, na hiyo ni sawa na kifo cha mtu mmoja kila baada ya sekunde sita.
Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Wanawake duniani kuna wanawake mbali mbali wanaojitoa kusaidia wanawake wenzao na wasichana. Miongoni mwao ni Marie Claudine Mukamabano kutoka nchini Rwanda ambaye anaishi Marekani. Marie ameanzisha kituo cha kuwalea watoto yatima nchini Rwanda.
Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na makundi mengine ya kiharakati pamoja na serikali ya Tanzania umeadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kupanda mlima kulimanjaro kama ishara mojawapo ya kusuma mbele nafasi ya mwanamke huku ikipinga vitendo vya dhulma dhidi yao.