Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 JULAI 2024

08 JULAI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi makubwa ya kijeshi nchini Ukraine yaliyotekelezwa na Urusi, na miradi ya maji nchini Sudan Kusini. Makala inamulika biashara kwa wakulima, vijana na wanawake, na mashinani inatupeleka nchini Ethiopia, kulikoni?

  1. Nchini Ukraine Jumatatu ya leo Julai 8 imeanza na wimbi jingine la mashambulizi makubwa ya kijeshi yaliyotekelezwa na Urusi na kuua makumi ya watu, hospitali ya watoto ikiwa ni miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa.
  2. Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Beth Bechdol amefanya ziara ya siku sita nchini Sudan Kusini na kuzindua miradi inayo saidia ukuaji wa kiuchumi huku ikipunguza migogoro na kuongeza uwezo wa wanachi kwenye kilimo.
  3. Katikamakala Assumpta Massoi akimulika mafunzo yaliyotolewa na mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na wadau ili kuimarisha biashara kwa wakulima, vijana, wanawake na wasimamisi wa mashamba ya kuzalisha mbegu mkoani Kigoma, kaskazini magharibi mwa Tanzania.
  4. Mashinani tutakupeleka Tigray nchini Ethiopia katika shule ya msingi ya Siye kusikia jinsi Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kwa ushirikiana na Muungano wa Ulaya lilivyoongeza kiwango cha uandikishaji na uhifadhi wa wanafunzi shuleni kupitia ukarabati wa madarasa na mpango wa mlo shuleni lakini kwanza ni makala.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
9'58"