Nchini Malawi mradi wa kusukuma maji kwa kutumia nishati ya jua au sola uliowezeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF umekuwa mkombozi kwa wanafunzi na jamii zinazozunguka mradi huo uliojengwa katika mkoa wa kati. John Kibego na maelezo zaidi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limewaondolea adha ya maji ya muda mrefu wakazi wa Paida jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambao walilazimika kutembea mwendo mrefu kusaka huduma hiyo muhimu kwa miaka mingi.
Mafuriko, mvua za kupindukia, ukame na kuyeyuka kwa barafu ni ishara kubwa ya mabadiliko ya tabianchi yanayohusisha maji limesema shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO.
Nchini Kenya ukuaji wa miji umekuwa na athari kubwa katika matumizi ya maji na usimamizi wa majitaka katika miji mingi, ambayo tayari inakabiliwa na ongezeko la mahitaji ya maji na huduma ya kujisafi, kwa mfano uchafuzi na matumizi kupitiliza.
Mradi wa maji safi na salama unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi kwenye makazi ya wakimbizi ya Bidibidi nchini Uganda umekuwa faraja sio tu kwa wakimbizi bali pia jamii zinazowahifadhi.
Mradi wa maji safi na salama unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi kwenye makazi ya wakimbizi ya Bidibidi nchini Uganda umekuwa faraja sio tu kwa wakimbizi bali pia jamii zinazowahifadhi.
Baada ya kughubikwa na vita kwa zaidi ya miongo mitatu sasa, ukame wa hivi karibuni umezidisha adha kwa mamilioni ya Wasomali ambao sasa wanahitaji huduma za msingi kama maji, malazi, huduma za afya na chakula.