Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Urusi

Mtazamo mpana wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati wanachama wanakutana juu ya vitisho kwa amani na usalama wa kimataifa.
UN Photo/Manuel Elías

Baraza la Usalama la UN lakutana kwa dharura kujadili tukio la ndege za kivita za Urusi nchini Estonia

Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa leo limeitisha kikao cha dharura kufuatia uvunjaji wa Urusi wa sheria za anga ya Estonia. “Ukiukaji wa sheria za anga za nchi huru haukubaliki.” Kauli hii ilitolewaleo kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu, Miroslav Jenča. Sababu ya kikao hicho ni tukio lililotokea Septemba 19, ambapo, kwa mujibu wa Estonia, ndege tatu za kivita aina ya MiG-31 za Urusi zilivunja sheria na kuingia katika anga yake.

© UNICEF/Oleksii Filippov

Vijana wengi zaidi wapoteza maisha na kujeruhiwa katika mashambulizi ya Urusi huko Ukraine: UNICEF

Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine yaliyofanyika usiku kucha, ikiwemo katika miji ya Kharkiv na Zaporizhzhia, yameripotiwa kuua watu 10 wakiwemo watoto watatu, kwa mujibu wa  taarifa  ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo. Flora Nducha na taarifa zaidi

Sauti
1'42"