Chuja:

Biashara

29 AGOSTI 2022

Flora Nducha anakuletea jarida lililo sheheni habari mbalimbali kuanzia nchini Ethiopia ambapo tume ya Kimataifa ya wataalamu wa Haki za binadamu nchini Ethiopia imekasirishwa na kuzuka upya kwa uhasama kati ya serikali ya Ethiopia na chama cha Tigray People's Liberation Front tangu wiki iliyopita na kuzitaka pande zote mbili kurudi kwenye meza ya mazungumzo kwani wanaoteseka ni raia.

Wakimbizi wa Burundi wakioko katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma nchini Tanzania wameshukuru kwa watoto wao kupatiwa vyeti vya kuzaliwa 

Sauti
10'26"

19 Mei 2021

Biashara ya bidhaa yapiga jeki uchumi wa dunia wakati wa COVID-19, imesema ripoti mpya iliyotolewa na kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD.

UNICEF Burundi yatoa mafunzo ya Ujuzi kwa Wasichana.

Na wakazi wakulima wa Keknaf, Bangladesh wanasema hata kabla ya kuja wakimbizi wa Rohingya, tayari wao walikuwa hoi, UNHCR imewasaidia. 

Sauti
13'4"
© FAO-Magnum Photos/Alex Webb

Nchi za Afrika ziko mbioni kuwa na soko moja la biashara:FAO/AU

Hii leo mjini Accra, Ghana, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO na Idara ya Kilimo, Maendeleo Vijijini, Uchumi wa Bahari na Maendeleo Endelevu ya Muungano wa Afrika, AUC-DARBE, wamezindua mwongozo wa kukuza biashara ya kilimo miongoni mwa mataifa ya Afrika chini ya makubaliano mapya ya Eneo la Biashara Huru barani humo,  AfCFTA. Anold Kayanda na taarifa zaidi

(TAARIFA YA ANOLD KAYANDA)

Sauti
3'28"

15 APRILI 2021

Katika jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika watia saini makubaliano ya kusongesha mkataba wa biashara huru barani Afrika ulioanza kutekelezwa rasmi mwaka huu wa 2021

-Nchini Burkina Faso adha ya wazazi wanawake kushindwa kufanyakazi kutokana na kukosa walezi wa watoto imepata dawa baada ya Benki ya Dunia na UNICEF kuanzisha mradi wa vituo vya kulelea watoto

Sauti
14'41"
WFP/Henry Bongyereirwe

Tumaini katika biashara ya mkimbizi kati ya changamoto za COVID-19, Uganda

Licha ya changamoto za biashara kudorora kutokana na vikwazo vya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona au COVID-19, wanawake wakimbizi nchini Uganda wanajitahidi kuendelea kujikimu wakiwa na matumaini siku moja mambo yatarejea kuwa kama kawaida. Basi ungana na John Kibego aliyetembelea jamii ya wakimbizi na kuzungumuza na mkimbizi mjasiriamali kutoka Rwanda.

 

Makala hii imetayarishwa na John Kibego

Sauti
3'27"