Wanawake wa Dodoma Singida na Zanzibar kunufaika na mradi wa pamoja wa UN
Hii leo Jumatano visiwani Zanzibar nchini Tanzania, mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la Chakula na Kilimo (FAO), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na kushughulikia masuala ya wanawake, (UN Women) wamezindua programu ya miaka mitano ya kuongeza kasi ya Uwezeshaji wa mradi wa uimarishaji uchumi wa wanawake wa Vijijini. Leah Mushi na taarifa zaidi.
(Taarifa ya Leah Mushi)