Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IMF yasema uchumi wa dunia bado umedorora

Shirika la fedha duniani IMF kupitia taarifa yake kuhusu mapato ya serikali na maendeleo ya kifedha iliyotolewa leo limeonya kwamba uchumi wa dunia unazorota wakati huu ambapo mazingira ya kifedha kote duniani yanaendelea kuwa magumu. Taarifa zaidi inasomwa na Happiness Palangyo wa redio washirika Uhai FM ya Mkoani Tabora Tanzania. 

(TAARIFA YA HAPPINESS PALANGYO) 

Akizungumzia hali hiyo mkutrugenzi wa idara ya masuala ya mapato ya serikali na fedha wa IMF mjini Washington DC Victor Gaspar amesema kushuka kwa kasi kwa uchumi kunaweza kuzidisha ubadilishanaji kati ya vipaumbele shindani vya usimamizi wa mahitaji, uimarishaji wa madeni, ulinzi wa watu walio katika mazingira magumu, na uwekezaji kwa siku zijazo. 

Ameongeza kuwa  

"Mkurugenzi mkuu ameeleza kwamba tunaishi katika ulimwengu dhaifu na wenye mshtuko. Taarifa ya mapato ya serikali inachunguza kwa kina jinsi sera za fedha zinavyoweza kuchangia katika jamii zenye mnepo ambapo watu wanaweza kurudi kujikwamua tena.” 

Taarifa hiyo imeendelea kusema kwamba deni la serikali la kimataifa linakadiriwa kuwa asilimia 91 ya pato la taifa mwaka 2022, ambayo ni asilimia 7½ juu ya viwango vya kabla ya janga la coronavirus">COVID-19, licha ya kupungua kwa uwiano wa hivi karibuni kwa nchi nyingi.  

Imeongeza kuwa madeni yalipungua kwa sababu ya kupunguza pengo lililokuwepo, kuimarika kwa uchumi, na majanga ya mfumuko wa bei. 

Bwana Victor akaenda mbali zaidi na kuweka bayana kwamba  

“Hatari kubwa inayosisitizwa katika taarifa hiyo ya mapato ya serikali ni madeni. Maendeleo ya hivi karibuni ya soko yanaonyesha kuongezeka kwa unyeti hadi kwa msingi dhaifu au kuzorota kwa misingi ambayo inaongeza hali ya mara kwa mara ya mizozo au kusambaa kwa matatizo yakifedha.” 

Mkurugenzi huyo amesisitiza kwamba kufafanua mfumo thabiti wa sera za muda wa kati kwa ulimwengu wa baada ya janga la COVID-19 ni muhimu.  

Pia amesema kutegemea mshangao wa mfumuko wa bei unaorudiwa ili kupunguza deni la umma sio mkakati mzuri na itasababisha shinikizo la matumizi kwa mfano, mishahara na gharama ya huduma.  

Mbali ya hayo amesema kupunguza pengo kama vile masoko mengi ya juu na yanayoibukia kunatarajiwa kuleta mabadiliko, na ni muhimu ili kusaidia kukabiliana na mfumuko wa bei na kushughulikia udhaifu wa madeni. 

"Taarifa ya ufuatiliaji wa mapato ya serikali inapendekeza utozwaji wa kodi kwa msingi wa haki. Mifumo dhabiti na mipana ya hifadhi ya jamii, kujenga akiba ya fedha, na kurejea kwa sheria za fedha,”  

Pakua

Shirika la fedha duniani IMF kupitia taarifa yake kuhusu mapato ya serikali na maendeleo ya kifedha iliyotolewa leo limeonya kwamba uchumi wa dunia unazorota wakati huu ambapo mazingira ya kifedha kote duniani yanaendelea kuwa magumu. Taarifa zaidi inasomwa na Happiness Palangyo wa redio washirika Uhai FM ya Mkoani Tabora Tanzania. 

(TAARIFA YA HAPPINESS PALANGYO) 

Akizungumzia hali hiyo mkutrugenzi wa idara ya masuala ya mapato ya serikali na fedha wa IMF mjini Washington DC Victor Gaspar amesema kushuka kwa kasi kwa uchumi kunaweza kuzidisha ubadilishanaji kati ya vipaumbele shindani vya usimamizi wa mahitaji, uimarishaji wa madeni, ulinzi wa watu walio katika mazingira magumu, na uwekezaji kwa siku zijazo. 

Ameongeza kuwa  

"Mkurugenzi mkuu ameeleza kwamba tunaishi katika ulimwengu dhaifu na wenye mshtuko. Taarifa ya mapato ya serikali inachunguza kwa kina jinsi sera za fedha zinavyoweza kuchangia katika jamii zenye mnepo ambapo watu wanaweza kurudi kujikwamua tena.” 

Taarifa hiyo imeendelea kusema kwamba deni la serikali la kimataifa linakadiriwa kuwa asilimia 91 ya pato la taifa mwaka 2022, ambayo ni asilimia 7½ juu ya viwango vya kabla ya janga la COVID-19, licha ya kupungua kwa uwiano wa hivi karibuni kwa nchi nyingi.  

Imeongeza kuwa madeni yalipungua kwa sababu ya kupunguza pengo lililokuwepo, kuimarika kwa uchumi, na majanga ya mfumuko wa bei. 

Bwana Victor akaenda mbali zaidi na kuweka bayana kwamba  

“Hatari kubwa inayosisitizwa katika taarifa hiyo ya mapato ya serikali ni madeni. Maendeleo ya hivi karibuni ya soko yanaonyesha kuongezeka kwa unyeti hadi kwa msingi dhaifu au kuzorota kwa misingi ambayo inaongeza hali ya mara kwa mara ya mizozo au kusambaa kwa matatizo yakifedha.” 

Mkurugenzi huyo amesisitiza kwamba kufafanua mfumo thabiti wa sera za muda wa kati kwa ulimwengu wa baada ya janga la COVID-19 ni muhimu.  

Pia amesema kutegemea mshangao wa mfumuko wa bei unaorudiwa ili kupunguza deni la umma sio mkakati mzuri na itasababisha shinikizo la matumizi kwa mfano, mishahara na gharama ya huduma.  

Mbali ya hayo amesema kupunguza pengo kama vile masoko mengi ya juu na yanayoibukia kunatarajiwa kuleta mabadiliko, na ni muhimu ili kusaidia kukabiliana na mfumuko wa bei na kushughulikia udhaifu wa madeni. 

"Taarifa ya ufuatiliaji wa mapato ya serikali inapendekeza utozwaji wa kodi kwa msingi wa haki. Mifumo dhabiti na mipana ya hifadhi ya jamii, kujenga akiba ya fedha, na kurejea kwa sheria za fedha,”  

Audio Credit
Flora Nducha / Happiness Palangyo
Audio Duration
2'54"
Photo Credit
ILO/K.B. Mpofu