Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yajipanga kuleta mabadiliko katika sekta ya Afya mwaka huu

Nusu ya idadi ya watu duniani bado wanakabiliwa na ukosefu wa huduma muhimu ya bima ya afya. Picha: World Bank

WHO yajipanga kuleta mabadiliko katika sekta ya Afya mwaka huu

Mkurugenzi wa shirika la Afya ulimwenguni WHO Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus amehutubia bodi ya shirika hilo hilo hi leo mjini Geneva katika hafla ya ufumbuzi wa kikao cha 142 cha bodi ya uongozi wa WHO .

Mkurugenzi wa shirika la Afya ulimwenguni WHO Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus amehutubia bodi ya shirika hilo hilo hi leo mjini Geneva katika hafla ya ufumbuzi wa kikao cha 142 cha bodi ya uongozi wa WHO .

Katika hutuba yake bwana Tredros amepongeza juhudi la shirika la WHO , chini ya uongozi wa kuleta  mabadiliko ya usawa wa kijinsia katika viwango vya uongozi wa WHO, kwa kuwa amini wanawake katika nafasi muhimu na nyeti  jambo ambalo ni hitoria katika uongozi wa shirika hilo.

Bwna Tedros  amepongeza  pia jitihada za WHO kuleta hamasa na mabadiko katika  serikali za nchi nyingi uilimwenguni, asasi za kiraia na mashirika ya kibindamu katika swala la huduma ya afya kwa wote akisema..

(Sauti ya Tedros)

"Tumeanza mchakato mpya wa kujumuika pamoja na  mashirika ya kiraia ili kuongeza sauti zetu za pamoja ambazo ni nguvu zaidi kuliko ile iliyogawanyika. Na tumekamilisha mwaka  sasa kuhusu makubaliano ya Tokyo kuhusu huduma ya afya kwa wote ambako tulishuhudia ahadi isiyokuwa ya kawaida kwa vyongozi wa kisiasa  katika kuunga mkono maono yetu ya afya kwa wote"

Na kuhusu jitahada za WHO kutokomeza magonjwa yasio ambukizwa Dr. Tedros alisema...

"Kwa kasi kubwa Tumeanzisha Tume ya ngazi ya  Juu itakayotuwezesha kukabiliana na  magonjwa yasiyoambukizwa  na pia  TB, ambayo yote yamepewa nafasi ya juu kushughuikiwa katika katika mkutano mkuu wa  Baraza kuu la Umoja wa Mataifa baadaye mwaka huu"