Skip to main content

UM wazindua kitabu kuhamasisha vijana kuhusu malengo ya milenia

UM wazindua kitabu kuhamasisha vijana kuhusu malengo ya milenia

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, shirika la mazao na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO pamoja na shirika la kupambana na ugonjwa wa ukimwi UNAIDS yameshirikiana katika uzinduzi wa kitabu cha vichekesho kilicho na lengo la kuwamasisha vijana walio kati ya miaka 10 na 14 kuhusu alengo ya milennia.

Uzinduzi huo utaongozwa na mshauri wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya michezo , maendeleo na amani Wilfried Lemke na unaambatana na uteuzi wa mlinda lango wa Hispania kama balozi mwema wa shirika la UNDP. Kitabu hicho chenye kurasa 32 kitatumia mchezo wa kabumbu na wachezaji wake manyota kuhamasisha na kitakuwa kwenye tovuti hii leo kama anavyoeleza bwana Lemke.

(SAUTI YA ANTOINE TAD)