Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifijo na nderemo vyashamiri Bentiu wakati wa ziara ya mkuu wa UNICEF

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF Henriette H. Fore (kati). Picha: UM/Video Capture

Vifijo na nderemo vyashamiri Bentiu wakati wa ziara ya mkuu wa UNICEF

Amani na Usalama

Kufuatia uteuzi wake kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Henrietta Fore amefanya ziara huko Sudan Kusini.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF amehitimisha ziara yake huko Sudan Kusini ambako licha ya kushuhudia madhila yanayokumba watoto ikiwemo utapiamlo uliokithiri , ameleta faraja kwa familia zilizokuwa zimetengana na watoto watoto wao. Siraj Kalyango na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Siraj Kalyango)

Nats..

Nchini Sudan Kusini, katika moja ya miradi ya maji ya mto Nile, Henriette H. Fore, Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF akiwasili na kulakiwa kukagua mradi wa maji yanayotumiwa na wakimbizi wa ndani…

image
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, Henrietta H. Fore asikiliza simulizi kutoka wafanyakazi wa UNICEF katika hospitalini nchini Sudan Kusini. Picha: UNICEF/UN0156591/Prinsloo
Kutoka hapa alitembelea hospitali ya watoto ya Al Sabbah mjini Juba akashuhudia watoto waliokabiliwa na utapiamlo uliokithiri, wakipatiwa tiba kwa njia ya mpira..

Nats..

Alielezwa na wauguzi jinsi wanavyokuwa na mtihani kwani watoto wagonjwa ni wengi lakini nafasi ya matibabu ni ndogo.

Nats..

image
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, Henrietta H. Fore. Picha: UM/Video capture
Baada ya machungu ni faraja.. alipanda helikopta kuelekea Bentiu akiwa na moja ya mtoto aliyepotezana na wazazi wake kwa zaidi  ya miaka miwili kutokanana vita nchini Sudan Kusini..

Nats..

Wanawake katika kituo cha wakimbizi wa ndani cha Bentiu walishindwa kuficha furaha yao na kumbeba juu juu Bi. Fore!

Nats…