Chuja:

Juba

Mama na mwana wakipata matibabu katika kituo kinachofadhiliwa na UNICEF huko River Nile nchini Sudan.
© UNICEF/Lok Ying Lau

Wakimbizi wa ndani nchini Sudan wanataka amani ili warejee makwao: Turk

Wakati idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Sudan ikizidi kuongezeka ambapo mpaka sasa wamefikia milioni 3.7 na kati yao 200,000 wakiwa wamerekodiwa mwaka huu pekee Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amefunga safari mpaka nchi huko kwenda kuzungumza na wawakilishi wa wakimbizi, asasi za kiraia na serikali. Tuungane na Leah Mushi anayetujuza yaliyojiri katika ziara hiyo.

Sauti
2'37"
UNICEF/Shehzad Noorani

Mradi wa UNIDO umeniondolea Umasikini

Mradi wa kuwezesha wanawake nchini Sudan Kusini unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda UNIDO kwa ufadhili wa serikali ya Canada umekuwa mkombozi mkubwa hasa kwa wanawake wavuvi na wakulima nchini mjini Juba nchini humo sio tu kwa kuwawesha kulisha familia zao lakini pia kupambana na umasikini.

John Kibego anafafanua zaidi 

UNMISS\Nektarios Markogiannis

Zimamoto mjini Juba Sudan Kusini waishukuru UNMISS

Mamlaka mjini Juba Sudan Kusini zimeushukuru Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS ambao umetoa msaada wa magari mawili makubwa ya huduma za uzimaji moto katika nchi hiyo ambayo miundombinu yake na huduma za kijamii vimeharibiwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu kwa takribani miaka mitano. Taarifa inasomwa na Loise Wairimu.

Sauti
2'57"
Mlinzi wa kikosi cha kulinda amani Sudan Kusini kutoka China akiwa anashika doria mjini Juba.Picha
UNMISS(Picha ya Maktaba July 2018)

Idara ya zimamoto mjini Juba Sudan Kusini yaishukuru UNMISS kwa msaada wake wa magari

Mamlaka mjini Juba Sudan Kusini zimeushukuru Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS ambao umetoa msaada wa magari mawili makubwa ya huduma za uzimaji moto katika nchi hiyo ambayo miundombinu yake na huduma za kijamii vimeharibiwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu kwa takribani miaka mitano.

Sauti
2'57"
UNHCR/Rocco Nuri

UNMISS yaenda Yei kusikiliza maswaibu ya wakazi

Nchini Sudan Kusini, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo,  UNMISS umechukua hatua ya kufunga safari na kukutana na jamii hasa kwenye maeneo yenye mzozo ili kuweza kupata simulizi zao kuhusu vitisho ambavyo wanakutana navyo na hatimaye waweze kufahamu hatua mahsusi za kuepusha ghasia. 

Sauti
2'32"
UNMISS/ Beatrice Mategwa

Kandanda yawaleta pamoja vijana mahasimu Sudan Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umekamilisha ujenzi wa uwanja wa kandanda nje kidogo ya mji mkuu, Juba lengo kuu likiwa kuwaunganisha wanajamii kupitia michezo. Flora Nducha na taarifa kamili.

Katika uwanja wa mpira wa miguu nje ya mji mkuu wa Sudan Juba, mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu sasa imeanza, timu mbili kutoka klabu ya Kor Romla zinachuana katika uwanja huu mpya uliojengwa kwa msaada wa walinda amani wa UNMIS kutoka Thailand na Nepal.

Sauti
1'46"
Kituo cha Umoja wa Mataifa cha kulinda Raia, Wau, Sudan Kusini.
UN

Mahakama ya kuhamahama yapeleka haki Malakal, Sudan Kusini.

Kwa zaidi ya kipindi cha siku tatu, mahakama ya kuhamahama inayofadhiliwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, imekuwa katika mji wa Malakal  jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini ili kushughulikia kesi kadhaa zikiwahusisha watu ambao walitenda makossa makubwa yakiwemo kesi mbili za unyanyasaji wa kingono na moja ya unyanganyi kwa kutumia silaha.

Sauti
2'28"