Sudan Kusini ni hatari kwa watoa misaada-UNICEF

Hali ya sasa ya kiusalama nchini Sudan Kusini si shwari kwa wafanyakazi wanaotoa misaada.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, Henrietta H. Fore amesema hayo leo akieleza kuwa shirika lake pamoja na mengine ya misaada nchini Sudan Kusini yanafanya kazi katika mazingira hatari wakati wakitoa misaada muhimu inayohitajika kwa watoto pamoja na vijana.
Ameeleza kuwa mwaka uliopita pekee, wafanyakazi 28 wa kutoa misaada waliuawa, ilhali mashirika hayo yanaendelea kutoka misaada kwa watoto walio katika shida.
Pia alizungumza na kijana wa umri wa miaka kumi alielazimishwa kujiunga na kundi moja la wapiganaji.
Vile vile alipata wasaa kukutana na watoto wawili ndugu ambao walitenganishwa na wazazi wao wakati mapigano yalipolipuka Bentiu mwaka 2010.